INFORMATION DESK
Updated 08/02/2026
Ni sehemu maalum ya mawasiliano ambayo lengo lake kuu ni kutoa uelewa, elimu na mwongozo kwa wateja kuhusu huduma za FEDAG ONLINE STATIONER.
MAJUKUMU MAKUU YA INFO DESK
- Kutoa elimu kuhusu website ya manunuzi na inavyofanya kazi
- Kutoa taarifa ya bei na ofa mbalimbali zilizoko Fedag Online Stationer.
- Kutoa ushauri kwa mahitaji maalum ya mteja.
- Kupokea Maswali, Maoni na Malalamiko
JINSI INFO DESK INAVYOFANYA KAZI
- Huduma hii itapatikana wakati wa mikusanyiko ya watu wengi. Mfano: Vikao vya wazazi, Mahafali ya shule, mashindano ya michezo n.k.
- Mteja atafika kwenye dawati la huduma na kueleza shida yake
- Mteja atapewa majibu sahihi kulingana na hitaji lake.